DEBATE TONONOKA 2010 MUISLAM NA MKRISTO NI NANI ATAKAYEINGIA PEPONI (1)

Yesu katika Lugha ya Kiarabu haiitwi ISA. jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa na Imam Baidhwawi voI.1 ukurasa wa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe. Yaani Zeruzeru, kwa kiingereza Albino. Jina ili lina sabihana na kuwa karibu na jina la kiebrania la Esau ambaye alipozaliwa alikuwa Mwekundu mwili wote. Mwanzo 25:24. ISSA A.S : JINA ILI HALINA NGUVU WALA UWEZO WA KUOKOA BALI NI RANGI MBILI Katika Al-Lu’lu’war-Marjani, Juzuu na1, Hadithi na104 uk. 64 “ Hadithi ya Ibn Abbas (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema, “Nilimuona Musa (a.s) katika usiku wa Al-Isra, niliopelekwa,naye ni mtu mrefu, mwenye nywele za hudhurungi zimejikunjakunja kama mtu wa Shanua.Na nilimuona Isa (a.s), naye ni mtu wa wastani wa umbo, unaelekea kwenye wekundu na weupe, ana nywele zilizonyooka……” 4.Maana ya jina Yesu Jina Yesu linatokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘Iesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema “ Yasu.”kwa kiingereza ni ‘’Jesus’’ Maana yake “Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi”Soma aya hizi.. Mathayo 1:18-21 na Luka 2:8-11. Bwana maana yake Mungu ndiye mwokozi Isaya 43:6, 10-11. Katika Biblia ambayo ina jumla ya Surah 1189 aya 31,102 vitabu 66 39, Agano la kale na 27 agano jipya neno Mwokozi kiiengereza wanasema Saviour limetajwa mara 55. ikumbuke kwamba katika agano jipya jina Yesu au kiebrania Yehoshua kiarabu Yashua au Yasu limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226. zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na Sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa siyo Bwana Yesu. YESU KRISTO: JINA LAKE NI WOKOVU. Mdo 4:9-10,12 “ kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu,jinsi alivyoponywa, jueni nyinyi nyote na watu wote wa Israel ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye nyinyi mlimsulubisha, na Mungu alimfufua katika wafu kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu…………………….Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” Jina tulilopewa ni jina moja tu lenye wokovu la Yesu Kristo. Jina la Isa a.s lisilo na wokovu limehusishwaje na jina la Yesu Kristo wa Nazareth lenye wokovu? Mdo 16:31 “ Wakamwambia , Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka wewe pamoja na nyumba yako.”